SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 2, 2010

Wazanzibari waafiki mpango wa kuanzishwa serikali ya umoja wa kitaifa

Wananchi wa Zanzibar wameamua kupiga kwa wingi kura ya ndiyo,
kwa shabaha ya kuainisha mustakbali wa kisiasa visiwani humo. Khatib Mwinyichande Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC ameeleza kuwa, asilimia 66.4 ya wapiga kura wameunga mkono mabadiliko visiwani humo, yatakayopelekea kubadilishwa katiba na hatimaye kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kati ya vyama vya CCM na CUF. Mwinyichande amesema kuwa, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar litaketi kwa ajili ya kuifanyia haraka marekebisho ya katiba ya Zanzibar, kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Mara baada ya kutangazwa matokeo hayo, Ramadhan Saleh Feruzi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar amesema kuwa, matarajio ya Wazanzibari ni kuona uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa uhuru na amani na yakiwemo mashirikiano ya vyama vyote vya kisiasa visiwani humo. Kura ya maoni ilifanyika jana visiwani humo bila ya kutokea rabsha wala machafuko ya aina yoyote ile.

1 comments:

emuthree said...

Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime wakipatana unaenda kuvuna,........

Post a Comment