SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 2, 2010

Umoja wa Mataifa watoa wito wa kupelekwa misaada ya kibinadamu Pakistan
Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa nchi na mashirika mbalimbali kote ulimwenguni kujitokeza kwa wingi na kutuma misaada nchini Pakistan, ambako mvua kubwa inayoendelea kunyesha, imesababisha vifo vya zaidi ya watu 1000. Duru kutoka nchini humo zimeripoti kuwa, idadi ya walioaga dunia kutokana na mafuriko hayo imepanda na kufikia 1,300 huku maelfu ya wengine wakiwachwa bila makao. Shirika la Afya Duniani WHO linaendelea kutoa matibabu ya dharura kwa waathiriwa mjini Peshawar. Mapema leo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa itatuma misaada ya dharura kwa waathiriwa wa janga hilo. Idara ya Hali ya Anga nchini humo imesema, mvua hiyo inatarajiwa kuendelea kunyesha zaidi katika maeneo mbalimbali nchini Pakistan. Janga hilo la kimaumbile linaaminika kuwa kubwa zaidi kuwahi kuikumba Pakistan tangu mwaka wa 1929.

0 comments:

Post a Comment