Uzinduzi wa Kipindi Kipya Kabisa cha Take One Ndani ya Clouds TV
Mtangazaji
mahiri wa kipindi cha Jahaz,Ephrahim Kibonde akimfafanulia jambo
mtangazaji mwenzake wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marious huku wakiruka
hewani LIVE kupitia Clouds TV.
Mtangazaji
wa Kipindi cha Take One,ambacho kimezinduliwa jana mbele ya wageni
waalikwa mbalimbali,Zamaradi Mketema akifafanua jambo mbele yao na
pamoja na watazamaji wa Clouds TV waliokuwa wakitazama majumbani mwao
Mmoja
wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akizungumza LIVE
kupitia Clouds TV kuhusiana na uzinduzi wa kipindi hicho ambacho
kinaanza kwenda hewani mara moja kulia ni mtangazaji mashuhuri Ephrahim
Kibonde.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Clouds TV wakifutilia kwa makini uzinduzi wa kipindi
kipya kitakachojulikana kwa jina la Take One chini ya Mtangazaji wake
mahiri kabisa katika uga wa filamu hapa Bongo,Zamaradi Mketema.
Wadau
wako bize wakifuatilia kwa makini kipindi cha Take One wakati kikiruka
hewani Live kupitia Clouds TV kushoto ni Ben Kinyaiya na Abdallah mrisho
kutoka Global Publishers
Wasanii mbalimbali wa filamu wakifuatilia kwa makini kipindi hicho ambacho kwa asilimia kubwa kitahusu uga wa filamu hapa bongo.
Wageni
waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kipindi cha
kwanza cha Clouds TV kitakachohusu tasnia ya filamu kiitwacho Take
One,uzinduzi wa hafla hiyo imefanyika Mjengoni humo humo na ilikwenda
LIVE.Picha zote na Ahmed Michuzi
0 comments:
Post a Comment