UN yaeleza wasiwasi wake kuhusu shambulizi la Israel kusini mwa Lebanon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ana wasiwasi kuhusu mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa jioni ya jana na jeshi la utawala haramu wa Israel katika ardhi ya Lebanon.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema Ban Ki-moon ambaye yuko safarini nchini Japan ameelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi yaliyofanywa jana na utawala wa Israel huko Lebanon na amezitaka pande mbili kuwa na subira. Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo lilifanya kikao kujadili mapigano yaliyozuka jana kati ya majeshi ya Lebanon na Israe baada ya utawala wa Kizayuni kuingia katika ardhi ya Lebanon. Kikao hicho kimefanyika kwa wito wa mwakilishi wa Lebanon.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amesema wapiganaji wa harakati hiyo hawatasimama kama watazamaji tu iwapo utawala ghasibu wa Israel utashambulia tena ardhi ya Lebanon. Amesema kuwa Hizbullah itakata mkono wa Israel utakaoshambulia jeshi la Lebanon na kwamba wapiganaji wa Hizbullah wako tayari kwa ajili ya kukabiliana na wachokozi.
0 comments:
Post a Comment