SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, August 5, 2010


Mkutano Wa Mwaka Wa 48 Wa Umoja Wa Mashauriano Ya Sheria Kwa Nchi Za Asia Na Afrika
Viongozi wa Mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika kutoka Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Kutoka kulia(mstari wa kwanza) ni Mwanasheria mkuu wa Serikali Fredrick Werema, Naibu Mwanashera mkuu George Masaju na Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea.
Mwanasheria mkuu wa Malaysia na Rais wa mkutano wa mwaka wa 48 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) Bw. Abdul Gani Patail akiongea na washiriki wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wafuatilia mkutano huo leo.Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe(kushoto) na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo (kulia) wakipata maelezo ya vitabu mbalimbali vya sheria kutoka kwa Bw. Omary Mwinyihery Afisa Masoko wa kampuni ya uchapishaji wa vitabu vya sheria (LawAfrica Publishing Ltd) leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika.
Washiriki wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Aron Msigwa – Globu ya Jamii)

0 comments:

Post a Comment