
Habari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema kuwa zaidi ya watu 50 wanahofiwa kufariki dunia baada ya lori walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika Ziwa Tanganyika, mashariki mwa nchi hiyo. Victor Choma Choma afisa wa ngazi za juu katika eneo hilo amesema kuwa lori hilo lilikuwa likisafirisha bidhaa kuelekea Burundi. Miongoni mwa waliokuwa ni wafanyabiashara ambao bidhaa zao pia zilikuwa kwenye lori hilo. Baadhi ya mashuhuda wamesema kuwa lori hilo lilikuwa limebeba watu kupita kiasi haswa ikizingatiwa kuwa mizigo iliyokuwemo ilikuwa na uzito mkubwa.




0 comments:
Post a Comment