SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, August 25, 2010

Ajali ya ndege yaua watu 42 nchini China
Sample Image
Watu wasiopungua 42 wamefariki dunia baada ya ndege ya shirika moja la ndege la China kuanguka wakati ilipokuwa ikijaribu kutua katika hali mbaya ya hewa ya ukungu mzito, katika ajali kubwa zaidi ya anga kutokea nchini humo kwenye kipindi cha miaka sita iliyopita. Watu 54 wamenusurika katika ajali hiyo iliyopelekea ndege ya shirika la ndege la Henan iliyokuwa na abiria 96 kupasuka vipande vipande. Ajali hiyo imetokea kaskazini mashariki mwa mji wa Yichun ulioko kwenye jimbo la Heilongjiang. Kwa mujibu wa shirika la habari la China Xinhua, rubani wa ndege hiyo ni miongoni mwa manusura wa ajali hiyo, hata hivyo ameshindwa kuzungumza chochote hadi sasa kutokana na majeraha makubwa aliyopata usoni. Huku timu ya waokoaji ikiendelea kupekua mabaki ya ndege hiyo, majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali nne za mji huo wa Yichun. Hadi sasa chanzo hasa cha ajali hiyo bado hakijajulikana..

0 comments:

Post a Comment