SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, August 25, 2010

Wafanyakazi wa sekta ya umma Afrika kusini wakaidi amri ya mahakama

Sample Image

Wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Afrika Kusini wamekaidi amri ya mahakama ya kuwataka wasitishe mgomo na kurudi kazini mara moja na badala yake wameendeleza mgomo wao ambao umeingia siku ya saba hii leo. Polisi wamelazimika kufyatua risasi za mipira ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiziba barabara na hospitali mjini Johannesburg. Imeripotiwa kuwa takriban waandamanaji 60 wametiwa nguvuni na huenda wakapandishwa kizimbani kwa kuzusha fujo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.
Jumamosi iliyopita serikali ya Afrika Kusini ilifanikiwa kupata kibali cha mahakama kinachopiga marufu mgomo huo ambapo Wizara ya Huduma za Jamii ilipewa idhini ya kuwaachisha kazi wafanyakazi watakaokataa kurudi kazini.

0 comments:

Post a Comment