MH. RAIS JK ZIARANI RUKWA
Mama wa Waziri mkuu Alberina Kasanga akimzawadia kuku
JK alipowatemebelea nyumbani kwao eneo la Kibaoni,wilayani Mpanda,mkoa
wa rukwa jana mchana. Kulia ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda,Baba ya Waziri
mkuu mizengo Pinda
Akiwa pamoja na wazazi wa Waziri Mkuu mhehimiwa mizengo
Pinda huko nyumabni kwao Kibaoni, wilayani Mpanda,mkoa wa Rukwa jana
mchana.Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda(80) Baba wa Waziri Mkuu na
kulia ni Mama Albertina Kasanga(70) Mama wa Waziri Mkuu
Mtaalamu wa Maabara katika hospitali ya mkoa wa Rukwa
bwana Dodea Mlenda akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi
mashine mpya za kisasa za uchunguzi wa maradhi zinavyofanya kazi muda
mfupi baada ya Rais Kuzindua maabara ya kisasa katika hospitali ya mkoa
wa Rukwa jana asubuhi.Maabara hiyo ya hospitali ya mkoa wa Rukwa ni kati
ya maabara 23 zinazojengwa katika mikoa mbalimbali nchini kwa msaada wa
shirika la Abbott Fund lenye makao yake nchini Marekani.Kushoto ni
Mbunge wa Kwela Chrisant Mzindakaya na watatu kutoka kushoto ni
Mwakilishi wa Waziri wa Afya Dr.Pamela Sawa.
JK akikata utepe kuzindua ujenzi wa mitambo mipya ya
kuzalisha umeme mjini Sumbawanga jana asubuhi.Mitambo hiyo itauwezesha
mji wa Sumbawanga na wilaya za jirani kupata umeme wa uhakika.Watatu
kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja,wa kwanza kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO mhandisi Willoima Mhando na wane
kushoto ni meneja mahusiano wa TANESCO Badra Masoud.
michuzi blog




0 comments:
Post a Comment