SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, June 5, 2010

BREAKING NEWS...BWANA YUSSUF CHUCHU HATUNAYE TENA!

 Marehemu CHUCHU wa pili kutoka kulia mwenye cap akiwa na wenzie wa bodi ya Sauti za Busara
Yussuf Ahmed Alley AKA Bwan Chuchu amefariki dunia jijini Nairobi-Kenya. Chuchu alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya mwanzoni mwa 2000 na bendi yake ya Chuchu Sound,iliyokua na wakali kama Mao Santiago,Omary Mkali,Waziri Sonyo,marehemu Gabby Katanga na wengine kibao,hasa na kibwagizo cha ''EEH..KWAHERI'' kwenye miondoko ya mduara. Na mpaka anafariki alikua anamiliki studio ya Heartbeat Records na kituo cha redio cha Chuchu FM vyote vipo kisiwani Zanzibar,na haijajulikana mara moja chanzo cha kifo chake. Msiba upo Kisima Majongoo na Mazishi yanafanyika kwenye makaburi ya MwanaKwerekwe leo saa 10,kisiwani Zanzibar. 
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMIN!
Kusikia kimoja ya vibao vya Chuchu Sound BOFYA HAPA

HATIMAE CHUCHU AZIKWA LEO

Hali ndivyo ilikuwa kama unavyoona picha hiyo hao ni baadhi ya watu waliojitokeza kuusindikiza mwili wa Marehe Yussuf Alley Almaarufu Bwanchuchu
Mamia ya wananchi na wasanii nchini jioni hii wanahudhuria mazishi ya msanii maarufu wa Zanzibar Yusuf Ahmed Alley maarufu bwan’chuchu katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya magharibi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari Marehemu Chuchu amefariki dunia mjini Nairobi, Kenya alikopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kuugua kiasi ya mwezi mmoja uliopita.
Mwili wa msanii umerejeshwa mjini hapa ambapo taratibu za mazishi zilifanyika katika mtaa wa Kisima Majongoo na maziko yanafanyika jioni hii katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya magharibi.

Hatimaye ule wakati ulifika,ndege iliyobeba mwili wa Bwanchuchu ikawasili uwanja wa ndege wa Zanzibar kama tunavyoona hapo taratibu ndege hiyo ikitua.

Vilio na simanzi vilitawala uwanja wa ndege na hasa baada ya kufunguliwa kwa mlango wa ndege hiyo kama tunavyoona pichani baadhi ya ndugu wa marehemu hapo wakibubujikwa na machozi baada ya kipenzi chao kuwasili akiwa katika hali nyengine tofauti na ile tuliyoizowea, hapo ni maiti sasa.

Hawa ni miongoni mwa watu waliobaki nje kabisa wakiusubiri mwili wa marehemu.

Wengi hatukuamini lakini ndio hivyo kazi yake mola haina makosa, lakini mapaparazi kama kawaida yao huwa hawakosekani katika sehemu kama hizi kama unavyomuona jamaa huyo akihangaika na camera yake kuhakikisha kuwa anapata kumbukumbu nzuri ya kifo cha Bwanchuchu.
Safari ya kumpeleka mpendwa wetu ilianza kueleka makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.

Kila mtu alitamani kuligusa jeneza la marehemu wakubwa kwa wadogo agalau kuonesha heshima kwa mwenzetu aliyetangulia mbele ya haki.

Hakika ilikuwa ni huzuni kubwa kwa wadau mbali mbali wa habari na muziki nchini,hapo kwenye picha ni miongoni mwa wadau hao wakitafakari na kutoamini kilichotokea kutokana na ukarimu na ucheshi wa Bwanchuchu kwa kila mtu. 
24 SEVEN 365 INATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU.

0 comments:

Post a Comment