Meles Zenawi
Waziri Mkuu wa Ethiopia ameikosoa vikali serikali ya Misri kutokana na
kung'ang'ania msimamo wake wa awali kuhusiana na umiliki wa maji ya mto
Nile. Zenawi ameongeza kuwa, serikali ya Misri haiwezi kuizuia Ethiopia
kujenga mabwawa yatakayohifadhi maji yanayotoka Mto Nile. Zenawi
ameongeza kuwa, baadhi ya watu nchini Misri wanafikiri kwamba maji ya
Mto Nile ni milki ya nchi hiyo, na serikali ya Cairo ina haki ya
kuchukua uamuzi wowote kuhusiana na mgawo wa maji hayo. Ameongeza kuwa,
baadhi ya Wamisri wanaamini kwamba nchi ambazo ni chimbuko la mto Nile,
haziwezi kutumia maji hayo kwa vile ni masikini na hazina uthabiti.
Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, licha ya kuwa Ethiopia ni nchi
masikini lakini inaweza kutumia mali asili zake kwa ajili ya kuimarisha
uchumi na miundo mbinu yake. Nchi nyingine zinazopakana na maji ya mto
Nile zinataka yawepo makubaliano mapya ambayo yatakuwa na mgawanyo sawa
katika utumiaji wa maji ya mto huo mrefu zaidi barani Afrika.Radio Swahili.




0 comments:
Post a Comment