Akina mama
watatu wa Kimarekani ambao watoto wao wametiwa mbaroni baada ya kuingia
nchini Iran kinyume cha sheria, wameiomba serikali ya Marekani iwaruhusu
akina mama wa Kiirani waonane na watoto wao ambao wanashikiliwa nchini
humo. Sarah Shourd, Shane Bauer na Josh Fattal walitiwa mbaroni mwezi
Julai mwaka jana na kikosi cha usalama cha Iran baada ya kuingia kinyume
cha sheria kwenye ardhi ya Iran wakitokea kaskazini mwa Iraq. Akina
mama hao walionyesha furaha zao walipokutana na watoto wao, na
kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na muamala mzuri
waliouonyesha kwa watoto wao. Wakati huohuo, Haidar Muslihi Waziri wa
Usalama wa Taifa wa Iran amesema kuwa, raia hao watatu wa Marekani
wanaoshikiliwa nchini wanakabiliwa na tuhuma za kufanya ujasusi nchini. |
Thursday, May 20, 2010
Wamarekani waridhishwa na hali za watoto wao wanaotuhumiwa kwa ugaidi
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 20, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook

Akina mama
watatu wa Kimarekani ambao watoto wao wametiwa mbaroni baada ya kuingia
nchini Iran kinyume cha sheria, wameiomba serikali ya Marekani iwaruhusu
akina mama wa Kiirani waonane na watoto wao ambao wanashikiliwa nchini
humo. Sarah Shourd, Shane Bauer na Josh Fattal walitiwa mbaroni mwezi
Julai mwaka jana na kikosi cha usalama cha Iran baada ya kuingia kinyume
cha sheria kwenye ardhi ya Iran wakitokea kaskazini mwa Iraq. Akina
mama hao walionyesha furaha zao walipokutana na watoto wao, na
kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na muamala mzuri
waliouonyesha kwa watoto wao. Wakati huohuo, Haidar Muslihi Waziri wa
Usalama wa Taifa wa Iran amesema kuwa, raia hao watatu wa Marekani
wanaoshikiliwa nchini wanakabiliwa na tuhuma za kufanya ujasusi nchini. 

0 comments:
Post a Comment