
Hali ya
mchafukoge imeendelea kuikumba nchi ya Iraq ambapo watu 23 wameuawa na
wengine 55 kujeruhiwa baada ya gazeti lililokuwa limetegwa bomu kuripuka
katika mji wa Khales ulioko kaskazini mashariki mwa mji mkuu Baghdad.
Mlipuko huo uliotokea sokoni, umesabisha mauaji makubwa zaidi katika
kipindi cha wiki nzima iliyopita. Itakumbukwa kuwa Ijumaa iliyopita
miripuko miwili ilitokea katika mji wa Tal Afar na kupelekea watu 25
kuuawa na wengine 120 kujeruhiwa.
Machafuko yanaendelea kupoteza
maisha ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa
mafuta, ikiwa hivi sasa zaidi ya miaka 7 imepita sasa tangu nchi za
Magharibi zikiongozwa na Marekani ziivamie nchi hiyo mwaka 2003 kwa
kisingizio cha kutafuta silaha za maangamizi ya umati.
0 comments:
Post a Comment