
Ameongeza kwamba, baadhi yao wana hali mbaya sana kiasi kwamba wamelazimika kuomba-omba milangoni mwa nyumba za watu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni 7.8 nchini Niger wanahitajia msaada wa chakula. Serikali ya mpito ya Niger mwishoni mwa wiki ilitangaza kuanza operesheni ya kugawa chakula kwa karibu watu milioni 1.5 wanaokabiliwa na njaa nchini humo. Mawaziri wa nchi za Afrika Magharibi pia, siku ya Jumatano walikutana
katika mji mkuu wa Togo, Lome kujadili matatizo ya chakula katika nchi
hizo.
0 comments:
Post a Comment