SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, July 7, 2014

Rais Dr. Jakaya Kikwete afurahishwa na miradi ya Shirika la Nyumba (NHC)

1w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na David Shambwe Kulia Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC) na Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, Wakati alipowasili katika banda la (NHC) na kukagua, Kupata maelezo mbalimbali ya shughuli za miradi inayotekelezwa na shirika hilo. Wakati alipotembelea maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE) maarufu kama Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam. Yanayofikia tamati kesho jijini Dar es salaam , Katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).

2w1
Rais Dr. Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wa pili kutoka kulia ni Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa Mawasiliano NHC.
4w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika la Nyumba NHC kwenye maonyesho ya Sabasaba Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dr. Abdalla Kigoda na Nalindwa Norbert mmoja wa maofisa wa Shirika la Nyumba NHC.
5w
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwahudumia watu mbalimbali waliotembelea banda lao ili kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
6w
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa NHC , Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara (NHC) Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi , Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki na Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC).
7w
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara NHC Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi, Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC) na Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa (NHC) wakisubiri kuwasili kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete katika banda lao.
3w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wakati alipotembelea banda hilo.

0 comments:

Post a Comment