SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 4, 2014

January: Nagombea urais 2015 kutekeleza vipaumbele vinne

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
----
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ametangaza nia yake ya kuwania urais akisema huu ni wakati wa kupisha fikra mpya kuongoza dola, licha ya chama hicho kuzuia kutangaza nia na kupiga kampeni kabla ya muda.

Makamba, mmoja wa makada wa CCM walioonywa na chama hicho baada ya kutuhumiwa kuanza kampeni mapema, alijipigia debe kuwa iwapo atapitishwa na chama hicho, ataelekeza nguvu kwenye vipaumbele vyake vinne ambavyo ni ajira, huduma za jamii, uchumi imara na utawala bora.
Mbunge huyo wa Bumbuli alisema hayo akiwa Uingereza anakohudhuria mkutano wa sekta ya mawasiliano baada ya kuhojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza na baadaye kufafanua nia hiyo katika mahojiano na Mwananchi jana.
“Ni wakati wa fikra mpya kushika dola na mimi ninaona kwamba wazee wakae kando. Mfano awamu moja inapoondoka na wazee walioko katika mfumo wakae kando ili kupisha fikra mpya kuongoza dola,” alisema Makamba ambaye ana umri wa miaka 40.
Mwandishi huyo wa zamani wa hotuba za Rais Jakaya Kikwete, alisema hadi sasa ameshafanya uamuzi kwa asilimia 90 kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu kuliko zote nchini, bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo ambayo anaendelea kuyatafakari, kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita “ili nipate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hili”.

Alipoulizwa iwapo ameshawishiwa au kushinikizwa na watu au ni utashi wake binafsi, Makamba alisema kuwa yote ni mchanganyiko.
“Huwezi kuamka nyumbani na kusema unakwenda kugombea. Kuna msukumo wa wapambe wachache ambao ni lazima ukapime kwa makini kabla ya kuchukua hatua yeyote,” alisema.
“Nchi nzima unakuta inazungumza uwe rais, lazima upime na chagizo hizo ni za kweli au zinatoka wapi. Lakini unaposikia hadi viongozi wa dini, wanafunzi wa vyuo unapokwenda wanakuuliza jambo hilo hilo, unatakiwa utafakari.”
Aliongeza: “Mfano unakwenda Maswa (Shinyanga), Liwale (Lindi), Simanjiro (Kilimanjaro), Wete (Pemba) unaambiwa unafaa, ni muhimu katika hili lakini pia wazee, vijana, viongozi wa dini wanasema unafaa kuwaunganisha Watanzania wote ni jambo la kulitafakari na kulichukulia hatua.”Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.......

0 comments:

Post a Comment