Kuna magonjwa mengine yakikupata hujui hata namna ya kujitibu. Lakini
kwa kutumia vyakula na matunda unaweza ukashangaa namna ambavyo unaweza
kuliondoa tatizo ambalo pengine ulidhani halina tiba.
Katika
makala haya ya leo, nakuletea uwezo wa ajabu unaopatikana kwenye juisi
ya kitunguu maji (Onion) kama tiba. Kuna maradhi mengi yanayoweza
kutibika kirahisi kabisa kwa kunywa juisi ya kitunguu, vilevile kuna
maradhi mengi unaweza kujikinga nayo kwa kunywa juisi hii.
Yapo magonjwa mengi yanayoweza kutibiwa kwa juisi ya kitunguu, lakini
katika mfululizo wa makala haya ya leo, nawaletea machache yafuatayo:
TATIZO LA KUTOKA DAMU
Kuna ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa, tatizo
ambalo huwapata watu wengi hasa wale ambao huwa na matatizo ya kukosa
choo kwa muda mrefu kutokana na ulaji mbovu walionao. Lakini pia tatizo
hili huweza kuwapata pia hata wale wanaokula vyakula sahihi lakini hukaa
muda mwingi bila kufanya mazoezi.
Kwa kitaalamu ugonjwa huu hujulikana pia kama ‘Hemorrhoids’. Wako
ambao husikia maumivu makali na wako ambao hawasikii maumivu ingawa
hutokwa na damu.
Kwa utafiti na ushuhuda mbalimbali uliokwisha tolewa juu ya tatizo hili, mtu unaweza kupona kabisa tatizo hili iwapo utaliwahi, kwa kunywa juisi ya kitunguu kwa utaratibu maalum.
Kwa utafiti na ushuhuda mbalimbali uliokwisha tolewa juu ya tatizo hili, mtu unaweza kupona kabisa tatizo hili iwapo utaliwahi, kwa kunywa juisi ya kitunguu kwa utaratibu maalum.
JINSI YA KUANDAA
Awali ya yote, hakikisha unapata kitunguu halisi kilichotokana na
kilimo cha kawaida kabisa (Organic Faming). Natoa tahadhari hii kwa
sababu siku hizi kuna vitunguu kutoka China, ambavyo ni vikubwa na
vyeupe kuliko kawaida. Hivi ni feki, havina virutubisho asilia.
Chukua kitunguu kimoja, ondoa maganda ya juu kama unavyofanya wakati
wa kuandaa kwenye mboga. Kama una ‘blender’ au ‘Juicer’, katakata na
weka kwenye kifaa chako, weka maji robo kikombe na saga ili kupata
juisi. Kama huna vifaa hivyo, usikonde, chukua kinu, changanya maji
kidogo na twanga hadi kupata juisi.
Bila shaka juisi yako itakuwa ni mchanganyiko wa maji maji na vipande
vya vitunguu vilivyosagika, usichuje bali kunywa hivyo hivyo kiasi cha
glasi moja. Hakikisha unatengeneza juisi na kuinywa wakati huohuo,
haitakiwi kuwekwa kwa muda mrefu kwani itapoteza ubora.
Inashauriwa kunywa juisi hiyo asubuhi kabla hujala kitu chochote na
baada ya kunywa, unaruhusiwa kula mlo wako baada ya saa moja mpaka saa
mbili. Kama huna nafasi ya kunywa wakati wa asubuhi, unaweza kutengeneza
juisi hiyo usiku na kuinywa kabla ya kupanda kitandani kulala.
Itaendelea wiki ijayo.
Itaendelea wiki ijayo.