SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, March 18, 2014

Home Shopping Center (HSC) yamzawadia mshindi wa ‘Give a Way’

Nadhir akimkabidhi hundi mshindi
Meneja Mauzo na Masoko wa HSC, Nadhir Mubarak Bahayan akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa shindano la ‘Give a way’ Rehane Jaffer (kulia) yenye thamani ya sh 500,000.

Na Andrew Chale
KAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za majumbani na ofisini ya Home Shopping Centre (HSC) imemzawadia mshindi wake wa kwanza wa ‘pendezesha nyumba na HSC’ Rehane Jaffer hundi ya sh 500,000.
Shindano hilo linaendeshwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na limepewa jina la ‘Give a Way’.
Hundi hiyo ilikabidhiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Mauzo na Masoko wa HSC, Nadhir Mubarak Bahayan ambaye aliwataka watanzania kushiriki shindano hilo ambalo kila Ijumaa watakuwa wakijishindia sh. 500,000.
hundi
 “Wateja wetu wa HSC, wanatakiwa kujiunga kwenye mtandao wetu wa facebook na kisha kututumia picha walizopamba ndani ya nyumba zao zitokanazo na bidhaa zetu,” alisema Nadhir.
Alisema shindano hilo litaendeshwa kwa mwezi mzima wa Machi. Mshindi huyo aliipongeza HSC kwa shindano hio na kusema ni faraja kwake na familia yake.
Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa  muda wa mwezi mzima wa Machi huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza washindi na kukabidhiwa hundi siku inayofuata.
Nadhir aliwataka wateja wao kuwa natabia ya kutembea kwenye mtandao wa HSC,  na kushiriki
kupokea hundi
Rehane Jaffer akipozi na hundi.
kuchagua bidhaa
Rehane Jaffer akichagua bidhaa ndani ya duka la Home Shopping Centre.
jinsi ya kushiriki
Jinsi ya kushiriki.