Mrembo
wa Tanzania Happiness Watimanywa akikabidhi baiskeli kwa mwenyekiti wa
Chawawaki Bi. Reberata Jovin kwenye sherehe zenye lengo la kusaidia
kikundi hicho, ambazo zimeandaliwa na taasisi ya TWA.
Mshauri
nasaha na mtoa mafunzo wa CCBRT,Bi. Mgaya Mhamanda akiongea na kinamama
wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo
cha kigamboni(Chawawaki) kwenye sherehe ya siku wanawake Duniani, ambayo
iliandaliwa na taasisi ya wanawake wenye mafanikio Tanzania TWA.
Katibu
wa kikundi cha Chawawaki,Bi. Upendo Ikombe katikati akiwa na Miss
Tanzania Happiness Watimanywa (kushoto) na Bi. Grace Rubambeyi mshindi
wa tuzo za Twaa, kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani
zilizofanyika shule ya msingi Mji Mwema Kigamboni.
Kina
mama wa kikundi cha Chawawaki Kigamboni wakimsikiliza rais wa Taasisi ya
Wanawake wenye Mafanikio Tanzania TWA Bi. Irene Kiwia(hayupo pichani)
kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani yenye lengo la kusaidia
kikundi hicho.
=====****=====
Taasisi
ya wanawake wenye mafanikio Tanzania (TWA) imesheherekea siku ya
wanawake duniani na kikundi cha wanawake wenye watoto wenye ugonjwa wa
mtindio wa ubongo na mgongo wazi wa Kigamboni (Chawawaki), yenye lengo
la kusaidia wamama hao ili waweze kupata msaada kutoka serikalini na
taasisi mbalimbali.
Wamama
hao wanaomba msaada wa kujengewa jengo na vifaa vya mazoezi kwa ajili
ya watoto wao. Kwa sasa wanatumia darasa kwenye shule la msingi
Mjimwema, siku moja kwa wiki tu, ambayo haikidhi mahitaji yakuwahudumia
watoto wao. Kikundi hicho kina jumla ya watoto 117 ambao wanaletwa kila
ijumaa kwa ajili ya kufanyiwa mazoezi na CCBRT.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kikundi hicho Bi. Reberata Jovin,
ameiomba serikali, watu na taasisi binafsi, ziweze kusaidia kikundi cha
wamama hao ili wapate msaada. Aliendelea kusema, "Kutokana na mazingira
waliokuwa nayo kwa sasa kwenye shule hiyo, hayafai kuwahudumia watoto
hao kwa sababu ya kuchangia vyoo na chumba kidogo cha kufanyia
mazoezi".
Pia
alisema elimu inahitajika kwa jamii kuhusu kuondoa dhana ya unyanyapaaji
kwa watoto hao na wazazi. "Mfano tunapokua kwenye mabasi au kwenye
mikusanyiko wa watu, watoto wetu wanaonekana kama misukule. Na wazazi wa
kiume wana tabia ya kuwaachia mzigo wa kulea mtoto huyo kwa wamama peke
yao".
Wito;
naomba serikali iangalie jamii zenye watoto wenye matatizo kama haya,
iwajengee vituo maalum ili waweze kupata huduma bila tatizo.
"Nashukuru
Taasisi ya wanawake wenye mfanikio Tanzania (TWA) na CCBRT kwa kuwa
nasi bega kwa bega kusaidia watoto wetu". Alimalizia Bi. Reberata Jovin.
NA MATUKIO-MICHUZI BLOG
0 comments:
Post a Comment