Mjumbe
wa bunge maalumu la katiba Fahmi Dovutwa akichangia mada wakati wa
semina ya wajumbe hao ya kupitia vifungu vya rasimu ya kanuni juzi.Picha
na Silvan Kiwale.
Mjumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba,Fahmi Dovutwa alichafua hali ya hewa baada ya
kuvituhumu vyama vya CCM, Chadema na CUF kuwa ndiyo vinavuruga Bunge kwa
sababu ya misimamo yao.Hali hiyo ilitokea wakati mjumbe huyo akichangia mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge Maalumu la Katiba juzi.Dovutwa
alitoa shutuma hizo baada ya mjumbe mwingine, Julius Mtatiro kueleza
kuwa amepitia Rasimu ya Kanuni lakini hakuona mahali panapoeleza
mpangilio wa ukaaji wakati wa kupiga kura.
Hali hiyo
ilimfanya Dovutwa, kusimama na kutoa tuhuma kuwa baadhi ya wajumbe
wamehongwa na kwamba kuruhusu mpangilio maalumu ni kukaribisha
mgawanyiko.
Alisema kukaa kwa mpangilio huo kutawapa nafasi viongozi mbalimbali kushinikiza wajumbe wao katika maamuzi ya mambo mbalimbali.“Ukaaji
wa sasa umezingatia masilahi ya nchi, utashi na matakwa ya wananchi.
Watu wa CCM, CUF na Chadema ndiyo mnaharibu mkutano (Bunge),” alisema
Dovutwa.Dovutwa alisema vyama hivyo vinatofautiana katika masuala mbalimbali na misimamo yao ndiyo imetawala bunge hilo.
“Mnatulazimisha
tuwasikilize nyie tu. Kwa hiyo Mwenyekiti usikubali, kikao hiki
kizingatie masilahi mapana ya makundi mbalimbali,” aliongeza Dovutwa.
Baada ya
kutamka hilo, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kupitia Kanuni, Amon Mpanju
alisimama na kumtaka Kificho kulisaidia Bunge hilo kwenda na utaratibu
aliowatangazia juzi wajumbe, ambao wanatakiwa kuwasilisha hoja zao
kwenye kamati kisha kutolewa uamuzi.“Naomba
uamuzi ukishafanyika, kiti chako kisiruhusu mtu mwingine kuingilia
maana mchakato hautafika mwisho. Nawaomba wajumbe wenzangu tusilete
michango inayoweza kuleta hisia za mgawanyiko miongoni mwetu,” alisema
Mpanju.
Mtatiro
alisema hakupendezwa na mchango wa Dovutwa na kutahadharisha ukweli
hauwezi kukwepeka kwa kuwa kuna watu wanaotoka katika makundi
mbalimbali.
“Wakati
wa kupiga kura tunahitaji theluthi mbili ya wajumbe wa Tanzania Bara na
idadi kama hiyo kwa wajumbe kutoka Zanzibar kwa hiyo ili kurahisisha
kazi hiyo, wajumbe kutoka Zanzibar wakae upande wao na wale wa Bara
wakae upande wao,” alisema Mtatiro.Hata
hivyo, akijibu hoja hiyo mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kupitia Kanuni,
George Simbachawene alimtaka mjumbe huyo kusubiri maelezo juu ya kifungu
kinachoelezea jinsi ya upigaji wa kura.“Kikishatolewa
uamuzi ndiyo tutafanya uamuzi, lakini nadhani upigaji kura utaongozwa
na utaratibu maalumu. Sidhani kama mapendekezo ya Mheshimiwa Mtatiro
tunaweza kuyachukua maana hatujui jinsi gani tutapiga kura,” alisema.
0 comments:
Post a Comment