Afisa Mtendaji Mkuu wa BOL, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
…Akizindua rasmi huduma hizo.
Wanahabari wakishuhudia uzinduzi huo.
Balozi
wa kampuni hiyo hapa nchini ‘Mkwere Orijino’ (katikati) Abdullatif na
kulia ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo Afrika Mashariki, Brian Azemchap
wakiwa kwenye pozi la furaha baada ya uzinduzi.
Kampuni za simu nchini zimezidi kupata
changamoto baada ya kampuni mpya ya BOL Smart ‘Lets Talk' kuzindua
huduma zake hapa nchini ambazo zinaungana katika mtandao wa pamoja wa
nchini za Afrika Mashariki, Uganda, Burundi, Tanzania.
Akizungumza na wanahabari kwenye mkutano na
wanahabari uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani,
aliwataka wananchi kutumia mtandao huo wa gharama nafuu kuliko yote hapa
nchini na hivyo kuwakomboa watumiaji wa simu. Mteja wa mtandao huo
atatozwa shilingi 79 kila atakapopiga simu na kuzungumza kwa dakika
zozote anazotaka.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)