Katibu wa Bunge Maalum la Katiba-Yahya Khamis Hamad
--
Rais
Jakaya Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge Maalum la Katiba Machi 21, mwaka huu mjini
Dodoma.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa
ofisi za Bunge mjini Dodoma.
“Kwa
mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21 ,mwaka 2014 saa 10:jioni,
ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na kuketi katika
maeneo watakayoelekezwa saa 9:00 alasiri,” alisema Katibu huyo.
Aidha
Katibu huyo alisema ratiba ya shughuli hiyo itaanza na kikao cha Bunge saa 9:10
na baadae kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea Rais .
Aliongeza
kuwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, Rais Kikwete atapokewa na
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Naibu Katibu wa Bunge Maalum, ambapo
baadae ataelekea katika jukwaa maalum kwa ajili ya kupokea salamu za heshima na
kukagua Gwaride Maalum ambalo limeandaliwa na jeshi la polisi.
Baada
ya shughuli zote kufanyika katika viwanja vya Bunge kumalizika, utaratibu
umewekwa kwa viongozi kuingia Bungeni kwa maandamano maalum.
Viongozi
watakaohusika katika maandamano hayo ni Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na
hatimaye Rais Kikwete ambaye atafuatana na Mwenyekiti wa bunge
hilo.
Katibu
huyo aliwataja viongozi wegine walioalikwa kuwa ni viongozi wa kitaifa na
watendaji wakuu kutoka pande zote Muungano, viongozi wa kitaifa wastaafu,ambao
ni marais wastaafu kutoka pande zote za muungano, mawaziri wakuu wastaafu,
waziri kiongozimstaafu na maspika wastaafu.
Viongozi
wengine ni mama Maria Nyerere, Mama Shadia Karume na Mwenyekiti na wajumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Wageni
wengine walioalikwa katika utaratibu huo ni taasisi za dini,
zisizozakiserikali, tansia ya habari, vyama vyote vya siasa vyenye
usajili wa kudumu, taasisi za elimu, vyama vya watu wenye ulemavu,
wafanyakazi,wafugaji,wavuvi, wakulima na wawakilishi kutoka sekta binafsi.
Kwa
mujibu wa ratiba ya shughuli hiyo Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia bunge hilo
kwa muda wa saa moja. Hivyo shughuli hizo zitakamilika majira ya saa 12:00jioni.
Na Magreth Kinabo
Na Magreth Kinabo