Askari
Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam wakibeba maborota ya mitumba
ya nguo za ndani kama sidiria na chupi leo katika soko la Karume katika
operesheni ya kukataza kuuza nguo za ndani za mitumba ambapo operesheni
hiyo ikiendeshwa na shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Marobota
ya nguo za ndani yakipakizwa katika magari ya polisi leo wakati shirika
la viwango Tanzania Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini wakati
walipoendesha operesheni Kataza kuuza nguo za ndani ambazo
zishatumika(mitumba)
Askari Polisi wakiendelea na operesheni hiyo katika Soko la Karume huku wafanyabiashara wa Sokoni hapo wakishuhudia zoezi hilo
Magari
ya polisi yakiwa Yamebeba Marobota ya Mitumba ya Nguo za Ndani mapema
leo katika Soko la Karume katika Operesheni kataza kuuza nguo za ndani
za mitumba
Msafara
kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi kwaajili ya kupeleka
Mzigo uliokamatwa wa nguo za ndani zilizotumika almaarufu kama mitumba
kwaajili ya kuteketezwa na moto wakati wa operesheni kataza kuuza
mitumba ya nguo za ndani
Msafara
wa polisi ukielekea Kituo Cha Msimbazi mapema leo mara baada ya
Kukamata wafanyabiashara na bidhaa zao za nguo za ndani za mitumba
Msafara ukiingia Katika kituo cha Msimbazi
Mzigo Ukiwasilishwa katika kituo cha Polisi Cha Msimbazi Kwaajili ya kwenda kuteketezwa na Moto
Mmoja
wa Wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akishusha sidiria
za mitumba ambazo zimekamatwa leo katika operesheni kata kuuza nguo za
ndani za mitumba
Mzigo Ukishushwa mara baada ya kufikishwa katika Kituo Cha Polisi Cha Msimbazi
Afisa
Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukamata marobota ya
nguo za ndani ambazo zimeshatumika wakati Nguo hizo zilishapigwa
marufuku kuuzwa nchini.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
0 comments:
Post a Comment