SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, March 18, 2014

BENKI YA COVENANT YATOA MAABASI NA BAJAJI KWA WAJASIRIAMALI

Mwenyekiti wa  Benki ya  Covenant  Balozi Salome Sijaona  akimkabidhi  mratibu wa uhamasishaji wa vikundi vya Wilaya ya Temeke Bi.Tukae Kondo ufunguo wa pikipiki baada ya kuwapatia mikopo wajasiliamali mbalimbali.Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi imewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo na mitaji. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.

Mwenyekiti wa  Benki ya  Covenant  Balozi Salome Sijaona  akimkabidhi  Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano cha  Yombo Vituka cha jijini Dar es Salaam,Charles Rweyemamu  ufunguo wa gari aina ya basi lenye thamani ya shilingi Milioni 45 .Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja. Mkurugenzi Mtendaji wa  benki ya Covenat  Sabetha Mwambenja, akiwasisitizia  jambo juu  ya kurejesha mikopo baadhi ya wajasiriamali waliopata mikopo  ya pikipiki  iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasilia mali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo . Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Balozi Salome Sijaona. Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant  Sabetha Mwambenja akiongea na Waandishi wa habari  juu ya benki hiyo kutoa mikopo kwa wajasiliamali wadogo  nchini  ili waweze kujikwamua  kimaisha kwa kuwapatia mitaji  ambayo ilijumuisha  Basi la abiria ,pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam 18, Machi, 2014

====****====
Benki ya Covenant kwa kushirikiana na Umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini wamewawezeha wajasiriamali zaidi ya 60 kujikwamua kimaisha kwa kuwapatia mikopo ya mitaji ambayo imejumuisha, Basi za abiria, Pikipiki za miguu mitatu maarufu kama bajaji pamoja na pikipiki Ushirikiano utakaowezesha zaidi ya wajasiriamali wadogo takribani milioni 6.8 ambao wote ni wanachama wa chama hicho nchini.

Akizunumza wakati wa makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Balozi.Salome Sijaona  amesema kuwa benki yake imeendelea kuwapa kipaumbele watu wote wa chini ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki na sasa wamewekeza zaidi katika kuwawezesha wajasiriamali hao kwa kuwapatia mitaji endelevu itakayo wawezesha kuingiza kuwaingizia kipato moja kwa moja.

“Benki yetu iko katika msitari wa mbele kuwawezesha Watanzania na wajasiriamali ambao hawako katika sekta rasmi na hawajafikiwa na huduma za kibenki, katika kuhakikisha tunafikia malengo haya, tumeweza kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha tunafikisha huduma zetu kwa watu wote,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa.

“Siku ya leo, tumekabidhi basi kubwa kwa kikundi cha  Mshikamano cha Wilaya ya Temeke, pia tumetoa bajaji 8 kwa wajasiriamali 8 pamoja na pikipiki 4  maarufu kama boda boda kwa wajasiriamali wanne na tutaendelea kutoa kwa wengine zaidi.  Tunaamini kuwa kwa kuwapa mikopo ya aina hii tutawawezesha wajasiriamali kuweza kujiendeleza kwa manufaa na kubadilisha Maisha yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bi. Sabetha Mwambenja, amesema benki yake imekuwa msitari wa mbele katika kufanikisha agizo lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika kuhakikisha kuwa benki zote zinawapa kipaumbele Watanzania ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki hasa walioko maeneo ya nje ya miji ambao ni zaidi wote ambao wamefikiwa na huduma za kibenki hadi sasa.

“Tumewekeza nguvu zetu katika kuwafiki Watanzania walionje ya miji na wale ambao hawajafikiwa kabisa na huduma za kibenki na tunaamini kuwa kwa Ushirikiano wetu na Chama cha wajasiriamali wasio katika sekta Rasmi tunaweza kuyafikia malengo haya na kuwa benki ya mfano katika kutekeleza agizo la Mheshmiwa Rais.” Alisema Mama Mwambenja na kuongeza kuwa

“Ninatoa wito kwa Watanzania wote hasa wanawake kujiunga na huduma za kibenki katika benki yetu ya Covenant na tunawaahidi kuwa tutawaonesha njia ya mafanikio katika biashara na Ujasiriamali”, alisema Mama Mwambenja na kuhitimisha kwa kusema.

“Tunaendelea kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujiunga na huduma zetu hadi sasa tunazo akaunti za aina mbalimbali ambazo ni akaunti za akiba inayojumuisha akaunti ya Ahadi, Jerusalem, Tausi Women Entrepreneurs Account, Winner Junior account, Vikundi, Akaunti ya Akiba ya Bajaj, Akaunti ya Muda Maalum na nyinginezo na akaunti za biashara ni pamoja na akaunti binafsi na nyinginezo”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano Bw. Charles Ryeyemamu ambao ndio waliokabidhiwa basi kubwa la abiria alisema wamefurahi kupokea msaada huo mkubwa na wao wanauona kama fursa kubwa ya kujikomboa kiuchumi na kutoa ahadi kwa benki hiyo kuwa watalitumia vyema na kuwa mfano wa kuigwa.