Ripota
wangu wa nguvu Julius Chemitei kutoka Nairobi anaripoti kwamba Hakimu
na pande husika dhidi ya washukiwa wa shambulio la Westgate wametembelea
eneo la tukio kutekeleza amri iliyotolewa na hakimu mkuu Daniel Ojenja
wiki iliyopita kabla ya kesi hiyo kuahirishwa.
Hakimu Daniel Ochenje alizungumza na waandishi kwenye hii ziara na
kusema umuhimu wa ziara hiyo ni kuwezesha pande husika kupata taswira ya
eneo hilo wakati Mashahidi
wanapolihusisha eneo la tukio kwenye
ushahidi wao Mahakamani.
Mawakili wa washukiwa wanaendelea kusimamia kwamba wateja wao hawana
hatia yoyote na baada ya ziara hiyo walikua tayari kuendelea na
kushirikiana na Mahakama wakati wakisubiri uamuzi kutolewa.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 27 & 28 January 2014
wakati upande wa mashtaka ukitarajiwa kuwasilisha mashahidi wengine 28
ambapo hata hivyo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa mawakili wa upande
wa Washukiwa kwamba viongozi wa mashtaka hawajawapa taarifa za polisi
zilizoandikishwa na mashahidi.
Hawa ni baadhi wa washukiwa wenyewe wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio la Westgate.
NA MIRLADAYO>COM
0 comments:
Post a Comment