Mkurugenzi
Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akielezea jambo kwa Naibu
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika ya Kusini, Bi. Elizabeth
Thabethe (katikati) na Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania, Bw.
Thanduyise Chiliza (kushoto). Ujumbe wa maafisa mbalimbali uliitembelea
EPZA jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu
wa Kiwanda cha nguo cha Tanzania Tooku Garments Ltd, Bw. Rigobert
Massawe (wa pili kulia) wakitoa zawadi kwa Naibu Waziri wa Biashara na
Viwanda wa Afrika ya Kusini, Bi. Elizabeth Thabethe (kushoto) wakati
ujumbe huo ulipotembelea kiwanda hicho kilicho ndani ya eneo la EPZA
jana. Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Bi.
Radhia Msuya.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Uhusiano
wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika ya Kusini unazidi
kuimarika baada ya nchi hizo kufikia makubaliano ya kuunda vikosi kazi
katika nchi hizo ili kuimarisha mamlaka za ukanda maalum za uwekezaji
katika nchi hizo.
Hatua
hiyo imekuja baada ya ujumbe wa maafisa toka serikali ya Afrika ya
Kusini kutembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji (EPZA) jana
jijini Dar es Salaam.
Ujumbe
huo ulioongozwa na Naibu Waziri wan chi hiyo wa Biashara na Viwanda,
Bi. Elizabeth Thabethe ulikutana na viongozi waandamini wa EPZA na
kupata fursa ya kufahamu kuhusu mamlaka hiyo na jinsi inavyofanya kazi
hapa nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa EPZA, Dkt…..Meru alisema Afrika ya Kusini ni nchi yenye uchumi
mkubwa barani Afrika na kuwa Tanzania ina mengi ya kujifunza hasa jinsi
mamlaka ya uwekezaji katika maeneo maalum ya nchi hiyo inavyofanya kazi.
“Tumekubaliana
kuunda vikosi kazi katika nchi zetu ili vifanya kazi ya kuhakikisha
kuwa mamlaka zetu zinaimarisha ushirikiano na kuongeza uwekezaji katika
maeneo yetu,” alisema Dkt. Meru.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa Afrika ya Kusini imekubali kuisaidia Tanzania
kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika maeneo ya EPZA hasa
katika maeneo ya kuongeza thamani mazao ya kulimo na madini, kuunganisha
vipuri kama magari na maeneo mengine.
Kwa
upande wake, Bi. Thabethe alisema kuwa uhusiano kati ya nchi yake na
Tanzania ni wa muda mrefu na kwamba ni muhimu ukaimarishwa kwa faida ya
watu wa pande zote mbili.
“Ni
kupitia biashara na uwekezaji baina ya mataifa ya Afrika ndipo bara hili
litaweza kupiga hatua za kweli za maendeleo,” alisema.
Alisema
Afrika ya Kusini ina mengi ya kujifunza toka Tanzania na kuwa wako
tayari kuimarisha uhusiano huo wa kibiashara na uwekezaji.
Balozi
wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya alizitaka mamlaka za
nchi hizo kufanya kazi kwa karibu ili kufikia maendeleo endelevu.
“Kuna mengi ya kushirikiana na kufanyia kazi kwa faida ya watu wetu,” alisema.
Kwa kushirikiana na Afrika ya Kusini, EPZA itakuwa inaimarisha zaidi mafanikio iliyopata hadi sasa.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizopo, pamoja na kujiwekea malengo ya kuvutia mtaji
wa Dola za Marekani 300 milioni kwa mwaka jana, mamlaka hiyo iliweza
kuvuka lengo na kuingiza nchini mtaji wa jumla ya dola za Marekani 498
milioni nchini, ikiwa ni thamani ya fedha za wawekezaji walioingia
nchini kwa mwaka huo.
Pia
mamlaka hiyo ilikuwa imejiwekea lengo la kuzalisha ajira 5,200 kwa mwaka
jana lakini hadi kufikia mwezi Disemba jumla ya ajira 10,200 zilikuwa
zimezalishwa kutokana na uwekezaji mpya uliofanywa kupitia mamlaka hiyo.
Taarifa
zinaonyesha kuwa EPZA ilikuwa imejiwekea lengo la kuuza nje bidhaa
zenye thamani ya dola milioni 100 2013 lakini lengo lilivukwa na kufikia
dola milioni 105 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment