Muonekano wa Kitabu hicho
Leo,
katika Maktaba ya Jiji la Dar-es-salaam ambayo pia ni Maktaba Kuu ya
Taifa, Faraja Nyalandu ambaye ni Mkurugenzi katika taasisi yake ya Shule
Direct amekabidhi kitabu chake kipya cha “Unaweza” kwa ajili ya
wanafunzi watakaofika kwenye maktaba hiyo.
Kama
jina la kitabu hicho, “Unaweza” ni kitabu kinacholenga kusaidia
wanafunzi kujenga uwezo na maarifa ili kumudu masomo yao. Ili waende
shule kwa malengo na sio tu kwasababu ni wajibu. Waweze kuelewa namna za
kujifunza. Zaidi, wajue namna za kuelewa na umuhimu wa kujenga
ufahamu.
Faraja
Nyalandu amenukuliwa akisema, “Kitabu cha Unaweza, Mbinu Kumi za kumudu
masomo yako, kilizaliwa kwa sababu nimeona kuna haja ya wanafunzi
kuhimili changamoto za uanafunzi na kufanikisha vyema azma ya kwenda
shule”
“Tunajifunza kila siku, kuna wakati tunajua kwamba hapa sasa tunajifunza
na kuna wakati hatujui kwamba tunajifunza. Ni muhimu kujenga misingi
hii ya kujifunza mapema.”
Faraja
pia amepongeza wanafunzi wote wanaotambua umuhimu wa kutumia maktaba,
akisema ni mfano wa kuigwa. Aidha Faraja ametoa wito kwa watu mbali
mbali wenye mapenzi mema na elimu kufadhili upatikanaji wa kitabu cha
“Unaweza” kwenye maktaba nyingine za mikoa na wilaya.
Faraja
amesema asilimia 50 ya mauzo ya kitabu cha “Unaweza” yataenda Chuo cha
Ualimu cha Korogwe, hususan Chumba cha TEKNOHAMA kwa ajili ya kuboresha
upatikanaji wa elimu kwa kutumia teknolojia.
Faraja akimwonyesha mwanafunzi sehemu wa kusoma.
Faraja akizungumza.
Faraja Kotta akiwa na Jacqueline Ntuyabaliwe.
Faraja Kotta akiwa na rafikiye Nancy Sumari
Faraja akikabidhi kitabu kwa mmoja wa wanafunzi waliokuwepo kwenye uzinduzi.
Raraja Kotta akiwa na Mkutubi wa jiji Misekelo Mwalugelo
Wadau mbalimbali walihudhuria.
Watoto wa shule ya msingi walihudhuria uzinduzi huo
0 comments:
Post a Comment