SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, January 24, 2014

SHUGHULI MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE AKIWA MJINI DAVOS, USWISI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kilimo uliofanyika mjini Davos,Uswisi usiku wa kuamkia leo Januari 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza,Mhe. Nick Clegg wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Sheraton mjini Davos, Uswisi leo Janaury 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan  Bw. Hiroyuki Ishige katika hoteli ya Sheraton mjini Davos, Uswisi leo January 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan Bw. Hiroyuki  Ishige katika hoteli ya Sheraton mjini Davos, Uswisi leo January 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah mara baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji salama kwa miaka ijayo katika hoteli ya Derby,mjini Davos Uswisi Januari 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa mara baada ya kuhutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji nsalama kwa miaka ijayo katika hoteli ya Derby,mjini Davos Uswisi Januari 23, 2014.  Wa tatu kulia ni mcheza sinema maarufu wa Hollywood Matt Damon, ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya jamii. 
PICHA NA IKULU.

0 comments:

Post a Comment