Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (Kati kati) akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma
Katibu wa Chama cha Walimu Bw.Ezekiel Oluoch akitoa mchango wake mkutano huo Katibu wa TUGHE Bw. Ally Kiwenge akitoa maoni yake katika mkutano.
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akijitambulisha kwa wajumbe wa mkutano ika mkutano.
Moja kati ya mada zilizowasilishwa katika mkutano kuhusu muundo wa utumishi wa walimu unaotumika hivi sasa.
Katibu wa Sekretariati ya Ajira bw. Xavier Daudi akitoa mchango wake katika mkutano.
Katibu wa Bodi ya Mishahara Bi. Tamika Mwakahesya akitoa mchango wake katika mkutano.
Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma imeitisha Mkutano maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma ili kupata mrejesho kuhusu masuala yanayowagusa watumishi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akifungua mkutano huo mjini Dodoma amesema mkutano huo maalum unafuatia maagizo yaliyotolewa katika mkutano uliopita.
“Kati ya yale yaliyosisitizwa na kukubalika ni kuitisha Mkutano Maalum wa Baraza kwa ajili ya kujadili Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Walimu na masuala mengine muhimu yanayohitaji ushauri wa Baraza” Bw. Yambesi alisema.
Bw. Yambesi, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo alisema baraza limeundwa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma, Na. 19 ya mwaka 2003, ambapo jukumu lake kubwa ni kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na utumishi wao. Utumishi wa Umma unasimamiwa na sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali. Hivyo, Baraza linao wajibu wa kushauri kuhusu miongozo mbalimbali inayosimamia Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu Bw. Yambesi alisema serikali inapenda kupata maoni ya wajumbe wa baraza kuhusu Tathmini ya utekelezaji wa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa mwaka 2000 unaohusu watumishi wa umma kujiunga na Siasa.
Alifafanua kuwa kwa sababu tunatarajia kuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na huenda baadhi ya watumishi wa Umma wakapenda kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa ambapo utaratibu uliopo sasa uliandaliwa miaka kumi na tatu (13) iliyopita, hivyo kuwepo umuhimu wa kupima kama bado unakidhi matarajio.
Pamoja na wajumbe wa baraza, katika mkutano huo maalum ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi mbalimbali ndani ya Utumishi wa Umma.
0 comments:
Post a Comment