SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 17, 2013

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla afungua Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake jijini Dar es Salaam

  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla akiingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake Barani Afrika lililofanyika katika Hoteli ya Peacok  jana Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,  Profesa Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla (Kulia) wakati wa Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake lililofanyika jana  Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mfuko wa Anita Foundation Dr. Anita White.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla akifungua Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa katika kongamano hilo jana Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, anayefuata kushoto ni Mkuu wa Mfuko wa Anita Foundation Dr. Anita White, kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo, na anayefuata kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Shirika la Right to Play Afrika Bw.Denis Bright, waliosimama nyuma ni wachezaji wa Twiga Stars ambao pia wameshiriki katika Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment