SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 9, 2011

MH.BALOZI KALLAGHE ATUA READING TAYARI KWA ZIARA RASMI


URBAN PULSE CREATIVE inapenda kuwaleta video fupi ya ziara maalum ya Mh Balozi wetu Peter Kallaghe kuhusu mpango mzima wa ziara yake ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika katika mji wa Reading hapa UK na kukutana na watanzania.
Kwa mujibu wa ratiba yake leo Mh Ataanza kukutana na wafanya biashara pamoja na wajasilimali, vikundi mbalimbali vya kitanzania ili kujenga mahusiano mazuri ya karibu baina ya ubalozi na watanzania waishio hapa nchini uingereza ikiwa ni pamoja na kusikiliza matatizo yao na kutoa ushauri jinsi gani ya kukabiliana nayo pia kujua msimamo halisi wa kiserikali wa kuwasaidia watanzania waishio ughaibuni.
Baada ya hapo Jumuiya imeandaa hafla ya nguvu leo jumamosi jioni ikiwa ni ishara ya kumkaribisha balozi. Address ya ukumbi ni WYCLIFF 233 KINGS ROAD, READING RG1 4LS kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa sita usiku.

Tafadhali Zingatia Mda na mjulishe mwenzako,

Asanteni,

Urban Pulse Creative

Kwa niaba ya
TANZ-UK/ TA READING

0 comments:

Post a Comment