SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 9, 2011

BENDI YA EXTRA BONGO WAPATA AJALI . WAPATA AJALI .

Wanamuzki wa bendi ya Extra Bongo iliyo chini ya uongozi wa Kamalade Ally Choki, wamepata ajali mbaya alfajiri ya leo wakati wakitoka katika onyesho lao lililofanyika kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza jana usiku.Wamepata ajali baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongwa na gari aina ya Fuso.
Gari lililokuwa limewabeba wanamuziki hao limepata ajali hiyo maeneo ya mataa ya magomemi Mapipa na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Kwa mujibu wa kiongozi wa bendi hiyo Ally Choki wanamuziki hao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili huku wawili kati yao hali zao zikiwa mbaya.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape ahueni majeruhi waweze kupona na kurejea katika hali zao za kawaida.

0 comments:

Post a Comment