SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 9, 2011

GBAGBO AIDHIBITI TENA ABIDJAN

Bw.Alain Le Roy.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa vikosi vinavyomtii kiongozi Laurent Gbagbo wa Ivory Coast anayeng’ang’ania madaraka vimeudhibiti tena mji mkuu wa nchi hiyo wa Abidjan.
Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Alain Le Roy, ameonya kuwa vikosi vya Gbagbo bado vina vifaru na silaha nyingine nzito na kwamba wako umbali wa kilometa moja tu kutoka kwenye hoteli ambayo ndio makao makuu ya kiongozi anayetambuliwa kimataifa Bw. Alassane Ouattara.
Kiongozi Gbagbo amekataa kukabidhi madaraka kwa Ouattara tangu uchaguzi wa rais wa Novemba mwaka jana, na ameendelea kubakia katika handaki kwenye makazi yake mjini Abidjan, ambayo yamezingirwa na vikosi vya Ouattara.
WAKATI HUO HUO
Umoja wa Ulaya umekubalia kuondoa vikwazo dhidi ya Ivory Coast ikiwa ni pamoja na kuzuia bandari mbili muhimu.
Rais Ouattara aliutaka umoja huo kuiondolea vikwazo nchi hiyo ambayo ipo katika machafuko kwa lengo la kuirejesha katika hali yake ya kawaida.
Wadau tutaendelea kuwata taarifa zaidi kuhusiana na ajali hiyo ya ndugu zetu kadri tutakavyoendelea kuzipata.

MO BLOG inamuomba Mwenyezi Mungu awape ahueni majeruhi waweze kupona na kurejea katika hali zao za kawaida.
Na Mo Blog Team.

0 comments:

Post a Comment