SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, September 16, 2013

Tanzania yasaini Mkataba wenye Thamani ya sh. Bilioni 10.3 Kupambana na Malaria

 Katibu Mkuu  Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile akibadilishana mkataba na Balozi wa Uswisi nchini Oliver Chave baada ya kutiliana saini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 10.3 kwa ajili ya kusaidia Mradi wa Kupambana na Malaria Kitaifa(National Malaria Control Program) leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu  Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam baada ya Serikali ya Tanzania kutiliana saini mkataba wenye thamani ya shillingi  bilioni 10.3 kwa ajili ya kusaidia Mradi wa Kupambana na Malaria Kitaifa(National Malaria Control Program) na Serikali ya Uswisi,kulia ni Balozi wa Uswisi nchini Oliver Chave.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Donald Mmbando akiongea na waandishi wa habari baada ya Wizara hiyo kupokea msaada wenye thamani ya  shilingi bilioni 10.3  kwa ajili ya kusaidia Mradi wa Kupambana na Malaria Kitaifa(National Malaria Control Program) kutoka Serilikali ya Uswisi,kulia ni  Katibu Mkuu  Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile.
Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo

0 comments:

Post a Comment