Padri wa kanisa Katoliki Parokia ya
Cheju Zanzibar, Anselmo Mwangamba amejeruhiwa usoni na kifuani baada ya
kumwagiwa tindikali na Watu wasiojulikana katika maeneo ya mlandege
jioni ya jana, akiwa katika harakati zake kupata habai na kuwasaliana na
jamaa kupitia mtandao wa Internet katika Cafe ya Sunshine mlandege, kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisikia Padre hiyo akilalama kuwa
amamwagiwa kitu cha majimaji na kuomba msaada kwa wananchi wa eneo hilo,
na kupata msaada wa huduma ya kwanza kutoka kwa mfanyakazi wa Cafe hiyo
kwa kutowa maji baridi na kumwagiwa. kwa mujibu wa dada wa duka hilo
Padre huyu hufika hapo kila siku kupata huduma ya internet. Mkasa huo
umemfika baada ya kumalizi kupata huduma hiyo na kutoka nje akiwa katika
eneo hilo walitokea watu wasiojulikana na kumwagia kitu hicho
kinachodhaniwa na tindi kali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani
Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika
mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja
kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa
Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na
Watu wasiojulikana jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni Unguja
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani
Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana
na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa kwamba
zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa
Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na
Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni Unguja.
Picha na Ramadhan Othman,IKULU-Zanzibar
0 comments:
Post a Comment