Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tenkolojia Profesa Makame Mbawara akihutubia wakati kampuni ya Vodacom Tanzania, kampuni ya Samsung na Benki ya CRDB PLC walipokuwa wakizindua mpango wa ushirikiano wa kuwawezesha wateja wao kujipatia simu aina ya Samsung Galaxy S3, Samsung Galaxy note 2 na Samsung Galaxy note 10 kwa malipo ya awamu kati ya miezi 12 hadi miezi 24 ambapo wateja wa benki ya CRDB PLC watajipatia huduma hiyo katika duka lolote la Vodacom nchini. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (wa tatu kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbawara, Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galaxy S3, Samsung Galaxy note2 na Samsung Galaxy note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24. Kushoto ni Meneja wa huduma za kibenki wa CRDB, Farida Mbwana.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbawara akimsikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galaxy S3, Samsung Galaxy note2 na Samsung Galaxy note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24, kushoto ni Mkuu wa Vifaa vya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bw. Mgopelinyi Kiwanga.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji -Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Bw. Saugata Bandyadhiyay akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akigonganisha glasi na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (wa tatu kushoto), Meneja Mwandamizi wa Kampuni ya Samsung, Afrika Mashariki Simon Kariithi (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mwendeshaji, Undeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay, mara baada ya kuuzindua mpango wa ushirikiano wao, Dar es Salaam juzi, ambapo utamwezesha mteja kununua simu za Sumsung kwa malipo ya awamu.
0 comments:
Post a Comment