SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 8, 2012

Rais Jakaya Kikwete Amteua Bi Mwanahamisi Omari Kitogo Kuwa Msaidizi Wa Rais,Huduma Za Jamii

 Rais Jakaya Kikwete
--
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2012

0 comments:

Post a Comment