SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 30, 2010


Ethiopia yatiliana saini makubaliano ya amani na wapiganaji wa Ogaden


Serikali ya Ethiopia imetiliana saini makubaliano ya amani na wapiganaji wa jimbo la Ogaden wa Muungano wa Kupigania Ukombozi wa Magharibi mwa Somalia (UWSLF). Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande husika zimekubaliana kusitisha mapigano na kuwaachilia huru wafungwa wa pande mbili. Makubaliano hayo ya kusitisha uhasama yameelezwa kuwa yana nafasi muhimu katika mchakato wa amani nchini Ethiopia. Awali serikali ya Addis Ababa na kundi hilo la wapiganaji la United Western Somali Liberation Front (UWSLF) zilitiliana saini makubaliano ya kusitisha mapigano Aprili mwaka huu huko nchini Djibouti, makubaliano ambayo yaliandaa uwanja wa makubaliano haya ya mwisho. Hata hivyo kundi jingine la Harakati ya Ukombozi wa Ogaden ONLF linalopigania kujitenga eneo la Ogaden lenyewe limeyapinga makubaliano hayo na kusisitiza kuendeleza vita vyake dhidi ya serikali ya Ethiopia.

0 comments:

Post a Comment