Iraq yazidi kugubikwa na machafuko, kuundwa serikali bado ni kitendawili
Watu wasiopungua 21 wamepoteza maisha yao nchini Iraq baada ya miji kadhaa ya nchi hiyo kushuhudia wimbi jipya la mashmbulio ya kigaidi. Vyombo vya usalama vya Iraq vinaripoti kuwa, miji ya Baghdad, Nainawa na al-Anbar hapo jana ilishuhudia mashambulio makubwa ya kigaidi yaliyopelekea kwa uchache watu 21 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Taarifa zaidi zinasema kuwa, shambulio la kigaidi lililovilenga vikosi vya usalama katika kitongoji cha A'dhamiya limepelekea watu 16 kuuawa huku tisa kati yao wakiwa ni maafisa wa usalama. Aidha mlipuko wa bomu katika mji wa Mosul mkoani Nainawa umesababisha polisi wanne kuuawa na wengine wanane kujeruhiwa. Hayo yanajiri katika hali ambayo licha ya kupita miezi kadhaa tokea ulipofanyika uchaguzi wa bunge nchini Iraq, lakini hadi sasa nchi hiyo imeshindwa kuunda serikali mpya kutokana na hitilafu zinazotawala katika anga ya kisiasa ya nchi hiyo
0 comments:
Post a Comment