SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 8, 2012

Airtel Yashiriki Uwekaji wa Mkongo wa Mawasiliano kutoka Dar-Tanzania Hadi nchini Shelisheli (Seychelles).

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya ( wa nne kushoto) akisaidia kazi ya uwekaji  wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uwekaji huo ambao  Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake. Wengine ni mafundi na wawakilishi wa makampuni yanayosimamia mradi huo.
 Waziri wa Viwanda na Maliasili wa Seychelles, Peter Sinon (kushoto), wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia), mafundi na wawakilishi kutoka Seychelees na Tanzania wakionyesha kipande cha mkongo wa mawasiliano kama ishara ya uzinduzi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana.  Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
 Mafundi wakiwa kazini wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam hadi nchini Seychelles jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kushoto) na Meneja Mawasliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando wakijibu maswali ya wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana.  Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.

0 comments:

Post a Comment