SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 24, 2010


Lubanga kuendelea kusalia Kizuizini ICC

Thomas Lubanga
Thomas Lubanga
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, iliyo na makao yake mjini the Haque, imefutilia mbali agizo la kumuachilia huru kiongozi wa waasi nchini Congo, Thomas Lubanga.
Mapema mwezi huu, Majaji wa mahakama hiyo walisimamisha kesi dhidi yake na kusema ni sharti aachiliwe huru.Majaji hao walisema upande wa mashtaka ulikuwa umehujumu kesi hiyo na kwamba kesi hiyo haingelisikilizwa kwa njia huru na haki.Viongozi wa mashtaka walikata rufaa kupinga uamuzi huo na mahakama hiyo ya ICC sasa imesema Bwana Lubanga atasalia kizuizini hadi rufaa hiyo itakaposikilizwa.Lubanga anatuhumiwa kuwasajili watoto kama wanajeshi wake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo.Mshukiwa huyo amekana madai hayo.

0 comments:

Post a Comment