Waziri wa mambo ya nje wa Urusi
Sergei Lavrov amelaani hatua ya Ufaransa kuwapa silaha waasi wanopinga
utwala wa kanali Muammar Gaddafi.
Bw Lavrov anasema hatua hio ikiwa imedhibitshwa
ni kosa kubwa kwani imekiuka azimio 1970 la umoja wa mataifa ambalo
linazuia silaha kuingizwa nchini humo na pande zote husika kwenye mzozo
huo.
Operesheni ya NATO Libya
Umoja wa Afrika pia umelaani uaamuzi wa Ufaransa wa kuimarisha nguvu za kijeshi za waasi hao.
Mwenyekiti wa tume ya Umoja huo Jean Ping amesema kitendo hicho kinaweka eneo zima hatarini.
Waziri wa mambo ya nje wa urusi amepanga kukutana na mwenzake kutoka Ufaransa Alain Juppe mjini Moscow kudhibitisha suala hilo tete.
Serikali ya urusi ilisusia kupigia kura mswada uliowasilishwa kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa kuruhusu harakati za kijeshi nchini Libya.
Mzozo unaoendelea mjini Libya ndio umepewa kipa umbele katika mkutano wa viongozi wa Afrika unaoendelea nchini Equatorial Guinea.
Bw Ping amesema kuna uwezekano mkubwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka nchini humo sawa na hali iliyoko nchini Somalia.
Mwenyekiti wa tume hiyo ya Umoja wa Afrika amefahamisha BBC kuwa mpango wa amani uliyobuniwa mnamo mwezi March bado unazingatiwa.
Mpango huo unataka pande zote zisitishe mapigano ili mazungumzo ya amani yaweze kuanza.
Habari kwamba Ufaransa imedondosha silaha nchini Libya zilijitokeza kupitia gazeti la Ufaransa, Le Figaro la jumatano.
Gazeti hilo lilisema kuwa Ufaransa, nchi inayoongoza operesheni ya NATO nchini Libya haikufahamisha nchi wanachama wenzake kuhusu operesheni hio.
Uwamuzi huo ulifikiwa baada ya mkutano uliofanyika mwezi April kati ya Rais Nicolas Sarkozy na Mkuu wa vikosi vya waasi wa Libya Gen Abdelfatah Younis.
0 comments:
Post a Comment