Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ridhwan Kikwete akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya
kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo
Mgombea Ubunge
wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhwan
Kikwete akionesha fomu aliyochukua ya kugombea ubunge jimbo la hilo
kulia kwake ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo, Kongo Kamate na
Mbunge wa viti maalum wa jimbo la Charinze Subira Mgalu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akijaza fomu
ya kugombea jimbo hilo.
ya kugombea jimbo hilo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ridhwan Kikwete akiongozana na wanachama wa CCM kwenda kuchukua fomu
fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo.
--
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete achukua fomu katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi wilayani Bagamoyo na leo anatarajia kurudisha fomu hiyo.
Akisindikizwa
na mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM wa jimbo la Chalinze na
Bagamoyo, Ridhwani alimhakikishia ofisa wa uchaguzi wa wilaya ya
Bagamoyo Shija Andrew, kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na
kutoendesha kampeni za
matusi na vurugu.
matusi na vurugu.
Baada ya kuchukua fomu hiyo pamoja na nakala nyingine muhimu za uchaguzi aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake
kuelekea kwenye ofisi za CCM Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa habari.
kuelekea kwenye ofisi za CCM Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa habari.
Katika mazungumzo yake hayo Ridhwan alitajavipaumbele vyake kwa kuleta maendeleo kwa wakazi wa Chalinze ambapo
alisisitizia kuimarisha upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
alisisitizia kuimarisha upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
“Kama
mnavyofahamu kuwa Chalinze ni eneo ambalo linakabiliwa na
changamoto nyingi kama vile maji, umeme na hata suala zima la ajira kwa
vijana sasa pindi ambapo nikipata Ubunge kwangu mimi nitahakikisha kuwa
napunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo hilo”alisemaRidhwan.
Aliongeza
kuwa “Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali zinazowakuta wakazi wa
wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa sikushinikizwa ila ni kwa
matakwa yangu mwenyewe naona
kabisa kuwa nipo katika hali na nguvu ya kushirikiana na wananchi
kumaliza shida za Chalinze”.
Ridhwan
pia alisema kuwa atasaidia kutatua ugomvi wa mara kwa mara unaowakumba
wakulima na wafugaji na kuwataka wakazi wa Chalinze kumchagua kwa
kishindo. Wakati huo huo mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa
tiketi ya Chadema Matayo Torongey akizungumza baada ya kuchukua
fomu alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua
maisha ya wakazi wa Chalinze Leo Ridhwan anatarajiwa kurejesha fomu za kugombea ubunge katika ofisi ndogo za uchaguzi.
Uchaguzi wa jimbo la Chalinze unakuja kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ramadhan Bwamdogo aliefariki
Januari 22 mwaka huu.
Januari 22 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment