Ongezeko
kubwa la idadi ya watu nchini India imewalazimu maafisa wa Afya kuanza kampeni
mpya ya mpango wa uzazi.
Serikali
inawasiwasi kuhusu idadi kubwa ya watu
Mpango
huo mpya wa uzazi unanuia kuwashawishi wanawake na wanaume kukubali njia ya
kumaliza kabisa nguvu za mayai ya uzazi.
Wanaokubali
watapokea zawadi ya gari lipya miongoni mwa zawadi nyingine.
Tata
nano, ndio gari lenya bei rahisi sana duniani lakini kulingana na kampeni hiyo,
bila shaka kuna uwezekano likawa maarufu zaidi nchini India katika siku chache
zijazo.
Dakatri
Sitaram Sharma anatazamia kuwa huenda gari hilo likawa kishawishi tosha kwa
wakazi wa jimbo la Jhunjunu kujitokeza kufungwa kizazi.
Lengo
la Daktari Sharma ni kuwa jumla ya wanawake na wanaume elfu 20 watajitokeza
kufungwa kizazi.
Kwa
taarifa yako, gari sio zawadi tu itakayotolewa kwenye kampeni hiyo. Watakao
fika watapewa piki piki, televisheni na vifaa vya kisasa vya kusagia vyakula.
Mpango
huo hauja lenga tuu wakaazi wa jimbo hilo ambalo mara nyingi linakabiliwa na
ukame.
Serikali
ya India imekuwa ikitatizika na idadi ya raia wake ambayo inakuwa kwa kasi
sana.
Hofu
za utawala nchini India ni kuwa ifikiapo mwaka wa 2030, heunda idadi ya watu
walioko nchini humo ikazidi ile ya wachina.
Hata
hivyo hakuna uhakika kuwa kampeni hii itaungwa mkono kote nchini India.
Mwaka
wa 70 ilipojaribiwa, maelfu ya watu walijotekeza kisha serikali ikashindwa
kutimiza ahadi zake kitu kilicho wachukiza wengi ambao walidai kuwa serikali
ilikuwa imewalaghai.
0 comments:
Post a Comment