SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 15, 2013

CDRB BENKI TAWI LA MLIMANI CITY YATOA MSAADA WA MABENCHI YA KUPUMZIKIA HOSPITALI YA PALESTINA-SINZA

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango (kushoto), akimkabidhi msaada wa mabenchi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina  Sinza, Dk.  Benedict Luoga yaliyotolewa na Benki ya CRDB tawi la Mlimani City kwa ajili ya kupumzikia wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango (kulia), akimuonesha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina  Sinza, Dk. Benedict Luoga, mabenchi yaliyotolewa na benki ya CRDB tawi la Mlimani City kwa ajili ya kupumzikia wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina  Sinza, Dk.  Benedict Luoga akiangalia mabenchi yaliyotolewa na Benki ya CRDB tawi la Mlimani City. 
Sehemu ya msaada wa mabenchi yaliyotolewa na Benki ya CRDB.  
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina  Sinza, Dk. Benedict Luoga (wa pili kushoto) akizungumza naMkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango .
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina  Sinza, Dk.  Benedict Luoga akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango mara baada ya kukabidhi msaada wa mabenchi ya kupumzikia.
Maofisa wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango.
Uongozi wa Hospitali ya Palistina Sinza ukiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki ya CRDB baada ya kukabidhi msaada wa mabenchi ya kupumzikia.

Na Francis Dande
 
BENKI ya CRDB tawi la Mlimani City, imekabidhi mabenchi kwa ya kuumzikia wagonjwa katika hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar es salaam ikiwa ni uendelezaji wa mpango mkakati wa kusaidia huduma za jamii.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi mabenchi sita ya kisasa, Mkurugenzi  wa Tawi hilo, Allen Killango, alisema CRDB hutenga asilimia moja ya faida yake ili kusaidia maendeleo ya jamii katika afya, elimu na utunzaji wa mazingira.
 
Killango, alisema kwa mwaka 2013 CRDB imesaidia kuboresha mazingira ya hospitali ya Mkoa Morogoro kwa kukarabati wodi ya watoto, kuweka vitanda, mashuka, magodoro na vyandarua.
Alisema pia wameikarabati hospitali ya rufaa Mbeya, wodi ya wazazi Bugando ikiwemo kufanya kampeni ya kuboresha mazingira ya hospitali kwa kupanda miche ya miti.
“CRDB inaamini katika  afya na siha kwa wateja wake, hakuna taifa lolote duniani linaloendelea kama wananchi wake hawana afya njema au hawapati huduma za hakika za matibabu,”alisema.
Naye Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Benedict Luoga, alishukuru CRDB kwa masaada huo na kuzitaka taasisi nyingine kuwasaidia kwani wana mapungufu ya mashuka, vitanda na magodoro.
 
“CRDB tunaishukuru sana maana ni benki inayorudisha faida hivyo tumepokea kwa mikono miwili na tutayatunza mabenchi na kuhakikisha yanatumiwa na watu wengi zaidi,”alisema. 
Hadi sasa CRDB imeendelea kupanua mtandao wake kwa kufungua zaidi ya ATM 350 zinazopokea kadi za visa, ikiwemo Mastercard, ChinaunionPay card

0 comments:

Post a Comment