SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, September 22, 2012

REDDS MISS KIGAMBONI AWATOTOA KIMASOMASO KWA KUTWA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA TEMEKE.


Redds miss kanda ya temeke Edda Sylivester katikati akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Masumbigana kushoto na Flaviana Maeda kulia mara walipotangazwa kuwa Redds Miss Kanda ya Temeke kwenye fainali iliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA Hall usiku wa kuamkia Leo
Tano bora ya Redds miss kanda ya temeke wakiwa katika picha ya pamojawalipotangazwa kuwa Redds Miss Kanda ya Temeke kwenye fainali iliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA Hall usiku wa kuamkia Leo.Picha zote kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited
**==**
 Edda Sylvester ndiye mshindi wa Redd's Miss Temeke 2012, katika shindano lililofanyika usiku wav kuamkia jana kwenye Ukumbi wa PTA (Sabasaba Hall).

Licha ya kushinda taji hilo Edda amepata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's  Miss Tanzania na kujinyakulia kitita cha sh.milioni 1 na zawadi zenye thamaini ya  shilingi 500,000.

Edda ambaye ametokea katika shindano la kitongoji cha Kigamboni ataungana  na Flaviana Maeda kutoka Kurasini ambaye amenyakuwa nafasi ya pili na  kujichukulia kitita cha shilingi 800,000.

Mrembo Catherine Masumbigana amechukua mshindi wa tatu katika shindano  hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi 700,000. Warembo hao watatu wamepata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's Miss  Tanzania ambayo itashirikisha warembo 30 ambao watakaa kambini kwa muda  wa mwezi mmoja.

Warembo Jesca Haule ambaye alishika nafasi ya nne amejipatia kitita cha shilingi  400,000 na nafasi ya tano ilienda kwa Agnes Gudluck ambae amejipatia shilingi  300,000.

Washindi wote watatu kila mmoja atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na  viatu, vikiwa na thamani ya kila mmoja shilingi 500,000 kutoka katika Duka la  kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu cha Sh 150,000  kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda. 

Warembo wengine ambao walishiriki kutoka katika vitongoji vya  Kurasini,Kigamboni na Chang'ombe ambao ambao wameambualiwa kifuta jasho  cha shilingi 200,000 kila mmoja ni Angela Gasper, Khadija Kombo, Neema  Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace,  Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Katika shindano hilo washehereshaji walikuwa wasanii wanaong’ara katika  luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambao  walionekana kuvunja mbavu za mashabiki waliyoudhulia shindano hilo. Licha ya kuwepo kwa Mpoki na Steven Nyerere Bendi ya muziki Mashujaa  Wanakibega ambao waliweza kutoa burudani ya nguvu chini ya Rais wao Charles  Baba.

Taji la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa  Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo 
wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.


Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge,  Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile,  Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM. 


Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo  Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham  mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi  kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo,  Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam  Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.

0 comments:

Post a Comment