Mwanajeshi aliyeasi nchini
Thailand Khattiya Sawasdipol amefariki dunia baada ya kupigwa risasi
wakati wa maandamanao mjini Bangkok wiki jana.
Kumetokea mlipuko nje ya hoteli zilizo karibu na maeneo waliko waandamanaji hao.Kufikia sasa zaidi ya watu 30 wameuawa tangu kuzuka machafuko Alhamisi wiki jana.Jenerali Khattiya alipigwa risasi kichwani wiki jana wakati akifanya mahojiano na mwanahabari wa jarida la NewYork Times.
Taarifa zaidi zimesema mwanajeshi mmoja wa serikali ameuawa kwenye ghasia zilizotokea hii leo.Waandamanaji hao wa mrengo wa ''RED SHIRT'' wamekuwa wakiandamana mjini Bangkok kwa miezi miwili sasa.
Wanamtaka Waziri Mkuu Abhisit Vejjajiva kujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya.Tangazo la hali ya hatari limetolewa kwa mikoa 20 kote nchini Thailand ili kuwazuia waandamanaji zaidi kuelekea katika jiji kuu.
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment