SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 11, 2010

Roy Bennett aachiliwa huru Zimbabwe
Mahakama ya Zimbabwe imetupilia mbali mashitaka dhidi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Zimbabwe Roy Bennett. Mashitaka hayo yalikuwa madai ya kupanga njama za kumuondoa madarakani rais Robert Mugabe.
Roy Bennett
Roy Bennett akiwa na Morgan Tsvangirai.
Bw Bennett ni mshirika wa karibu wa Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.
Jaji wa mahakama amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa barua pepe zinazodaiwa kumhusisha bw Bennet na muuza silaha mmoja, zilikuwa halisi.
Kesi hiyo ilitishia kugawanya serikali ya umoja inayoongozwa na mahasimu wa muda mrefu, bw Mugabe na bw Tsvangirai.
Bw Bennett alikuwa nje kwa dhamana.
Bw Bennett ni kiongozi wa juu wa chama cha bw Tsvangirai, MDC, na alitakiwa kuchukua wadhifa wa naibu waziri katika serikali, wakati alipokamatwa mwezi Februari mwaka 2009.

0 comments:

Post a Comment