William Ngeleja waziri wa Nishati na Madini
---
Na Nova Kambota
---
Na Nova Kambota
Kama
kuna jambo linalowaumiza vichwa watanznia basi ni swali kuwa kwanini
kila wanalopanga halifanikiwi? au kwanini wananchi ni masikini licha ya
maliasili zilizojaa kila kona yanchi hii? Wakiangalia elimu hoi watoto
wanafeli, wakija kwenye afya hakuna kitu, wakienda kwenye kilimo na
hata umeme tabu tu kwa kifupi hakuna jipya ni uduni na ubabaishaji
mtupu.
Katika lindi la mawazo ya namna hii au maswali mengi yasiyojibika tunawatazama viongozi wetu na uwajibikaji wao usiokidhi viwango kiasi kwamba wamepwaya mno , wajuzi wa kuzungumza bila kutenda, ni watu wa blah blah na porojo tu.

Kwakweli Tanzania imetawaliwa
na wapiga porojo hebu angalia kwenye hiyo kaulimbiu ya “kilimo
kwanza”inavyotangazwa na kupigiwa chapuo na viongozi wetu kasha nenda
huko vijijini kwenye mashamba utaona hata mabwana shamba hakuna na hizo
pembejeo zenyewe za kilimo hakuna, sasa utasema hapo kuna kilimo
kwanza au porojo tu?
Geukia elimu nddio utashangaa kabisa kulivyooza huko lakini cha
ajabu ni kuwa viongozi wetu bado wna ujasiri wa kusimama kwenye majukwaa
na kudai kuwa serikali imeboresha elimu, elimu gani? Shule za kata? Si
ndio hizi zinatoa sifuri? Nasikia siku hizi zinaitwa mtambo wa sifuri,
ajabu sana! Yaani serikali inajenga majengo tupu bila walimu,madawati
wala maabara kasha wanaita sekondari halafu wanazidi kuboronga wanafuta
mitihani, tuziiteje hizi? Hizi ni porojo za watawala wetu, porojo
porojo kila mtu anapiga porojo tu.
Njoo kwenye hizo huduma za afya ,
tunaambiwa kuwa Tanzania bila maralia inawezekana tena kwa mbwembwe kwa
matamasha makubwa lakini hivi mtu wa kule kijijini analala chini hana
hata hiko kitanda je hiyo neti atachomeka wapi? Au motto wa mtaani
analala kwenye vichochoro huyu neti atachomeka wapi? Sasa hizo Zahanati
za vijijini kama kweli zinaviwango mbona vifo vya akina mama
wajawazito bado vinaendelea? Hakika hizi ni porojo za viongozi wetu!
Halafu anaibuka kiongozi mkubwa wa
nchi anadai msongamano wa magari jijini Dar es salaam ni ushahidi wa
kukua kwa uchumi wetu, hizi sasa porojo, uchumi wetu na nani? Mafisadi?
Au Brigedia Al Adawy na Dowans? Uchumi umekua na ombaomba wameongozeka
ndiyo magari yameongezeka na umasikini umekithiri , sasa huo uchumi
uliokua umemnufaisha nani? Mawaziri na wabunge? Au rais na waziri mkuu?
Hizi ni porojo tupu.
Serikali
nayo imeshindwa kuweka huduma za nishati ya umeme wa uhakika, sasa
naona ina mchoko naam! Huu ni mchoko ndio maana kila kwenye hotuba
tunapigwa kalenda mpaka mwaka huu au ule tatizo la umeme litakuwa
historia halafu mda huohuo umeme ni wa mgao, waziri wa nishati nay eye
hana jipya bado watu tunateseka kwa sababu ya kukosa ubunifu na
uzalendo , mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati anataka tuwashe
mitambo ya Dowans, watu wanahoji anataka turudi tulipotoka? Hizi kama
sio porojo nini basi? Nchi ipo gizani viongozi wanapiga porojo
inasikitisha sana.
Tabia ya kupiga porojo inaendelea
kudidimiza nchi , hata kwenye michezo tunapiga porojo halafu tunataka
kucheza kombe la Dunia,bungeni kuna porojo kiasi kwamba bunge
linafanywa sehemu ya kupigana vijembe na mipasho halafu na sisi
tunaamini iko siku tutakuwa kama wenzetu wa Ulaya na Marekani ambao
tayari wamefuta blah blah na porojo kwenye kamusi za vichwa vyao
wanafanya mambo kizalendo na kwa kujituma, haiwezekani!
Matokeo ya porojo yanapoonekana
viongozi wetu hawachelewi kusikitika na kuhidi kujirekebisha, ona
matokeo ya kidato cha nne yalivyowaumbua viongozi sasa wanajifanya
wamejifunza hakuna kitu porojo tu , mabasi yanakimbia yanavyotaka wenye
jukumu la kulinda usalama barabarani wanapiga porojo watu wanakufa
utadhani ni msimu wa ajali.
Siku hizi hadi viongozi wa dini wamekumbwa na tabia ya kupiga porojo , badala ya kutetea wanyonge wao wanagombana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kujigeuza miungu watu wanadanganya masikini na kuwakamua hata kidogo walichonacho na wengine wamejigeuza watabiri wanatabiria watu kufa? Hizi ni porojo tupu.
Sasa katika muktadha huu ndio maana najiuliza kuwa nchi hii iliyolewa kwa wingi wa porojo itaendelea vipi? Badala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma kwasababu ya porojo zisizokwisha na hazina mipaka hata kwenye mambo ya msingi tunapiga porojo au ndio tunategemea kuendelea kwa miujiza ya Mussa? Tafakari!

Nova Kambota Mwanaharakati,
0717 709618 au +255717 709618
Tanzania, East Africa,
June 30, 2011
CHANZO: H@ki Ngowi
0 comments:
Post a Comment