SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 30, 2011

Taswira Zaidi Za Ziara Ya Mama Salma Kikwete Huko Comoro

Mke wa Rais wa Mama Salma Kikwete(aliesimama kushoto)akiongea katika haffa ya chakula cha usiku Juni 28, 2011 huko Comoro.(wa pili kutoka kwake) ni Mke wa Rais wa Comoro Mama Hadidja Aboubacar Ikililoi .
Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha usiku Juni 28,2011 katika Ikulu ya Comoro, kilichoandaliwa na Mke wa Rais wa Comoro Mama Hadidja Aboubacar Ikililoi Dhoinine(hayupo pichani) kwa heshima ya Mke wa Rais mama Salma Kikwete
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(kushoto)akipokea zawadi kutoka kwa Mke wa Rais wa Comoro Mama Hadidja Aboubacar Ikililoi Dhoinine wakati alipomtembelea nyumbani kwake mjini Comoro na kubadilishana mawazo.(juni 28.2011)
Mke wa Rais mama Salma Kikwete(kushoto)akiagana na Rais wa Comoro Dr.Ikililoi Dhoinine alipomtembelae Ikulu Comoro na kuzungumza nae. Juni 28,2011.
Kikundi cha ngoma ya asili ya Comoro kikitumbuiza wakati wa hafla ya Chakula cha usiku alichoandaliwa mke wa rais mama Salma Kikwete na mwenyeji wake mama Hadidja Aboubacar Ikililoi Dhoinine Ikulu. June 28, 2011- 
(Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO)

0 comments:

Post a Comment